98Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu, kwa kuwa nimezishika daima.
99Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.
100Nina ufahamu zaidi kuliko wazee, kwa kuwa ninayatii mausia yako.
101Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, ili niweze kutii neno lako.
102Sijaziacha sheria zako, kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe.