Zaburi 119

Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.

Psalm 119:105 (UKJV) Your word is a lamp unto my feet, and a light unto my path.

103Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu!

104Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.

105Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.

106Nimeapa na nimethibitisha, kwamba nitafuata sheria zako za haki.

107Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Bwana, sawasawa na neno lako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.