146Ninakuita; niokoe nami nitazishika sheria zako.
147Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada; nimeweka tumaini langu katika neno lako.
148Sikufumba macho yangu usiku kucha, ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako.
149Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako, Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako.
150Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami, lakini wako mbali na sheria yako.