1Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya Bwana.
2Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote.
3Wasiofanya lolote lililo baya, wanaoenenda katika njia zake.
4Umetoa maagizo yako ili tuyatii kwa ukamilifu.