70Mioyo yao ni katili na migumu, bali mimi napendezwa na sheria yako.
71Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako.
72Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.
73Mikono yako ilinifanya na kuniumba, nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.
74Wakuchao wafurahie wanaponiona, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako.