8inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako.
9Makuhani wako na wavikwe haki, watakatifu wako na waimbe kwa furaha.”
10Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako, usimkatae mpakwa mafuta wako.
11Bwana alimwapia Daudi kiapo, kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua: “Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe katika kiti chako cha enzi,
12kama wanao watashika Agano langu na sheria ninazowafundisha, ndipo wana wao watarithi kiti chako cha enzi milele na milele.”