9Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri, dhidi ya Farao na watumishi wake wote.
10Aliyapiga mataifa mengi, na akaua wafalme wenye nguvu:
11Mfalme Sihoni na Waamori, Ogu mfalme wa Bashani na wafalme wote wa Kanaani:
12akatoa nchi yao kuwa urithi, urithi kwa watu wake Israeli.
13Ee Bwana, jina lako ladumu milele, kumbukumbu za fahari zako, Ee Bwana, kwa vizazi vyote.