15Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
16Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona;
17zina masikio, lakini haziwezi kusikia, wala hakuna pumzi katika vinywa vyao.
18Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
19Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana; ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana;