8Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi kuwa kitanda changu, wewe uko huko.
9Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko, kama nikikaa pande za mbali za bahari,
10hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti.
11Kama nikisema, “Hakika giza litanificha na nuru inayonizunguka iwe usiku,”
12hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utangʼaa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.