10Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! Na watupwe motoni, katika mashimo ya matope, wasiinuke tena kamwe.
11Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi; maafa na yawawinde watu wenye jeuri.
12Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki, na kuitegemeza njia ya mhitaji.
13Hakika wenye haki watalisifu jina lako, na waadilifu wataishi mbele zako.