8Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao, usiache mipango yao ikafanikiwa, wasije wakajisifu.
9Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe na shida zinazosababishwa na midomo yao.
10Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! Na watupwe motoni, katika mashimo ya matope, wasiinuke tena kamwe.
11Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi; maafa na yawawinde watu wenye jeuri.
12Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki, na kuitegemeza njia ya mhitaji.