1Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele.
2Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele.
3Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.
4Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu.
5Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.