3Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.
4Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu.
5Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.
6Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu.
7Wataadhimisha wema wako mwingi, na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.