13Bwana alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.
14Aliipiga mishale yake na kutawanya adui, naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza.
15Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwako, Ee Bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako.
16Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.
17Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.