31Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu?
32Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.
33Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu.
34Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.
35Hunipa ngao yako ya ushindi, nao mkono wako wa kuume hunitegemeza, unajishusha chini ili kuniinua.