32Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.
33Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu.
34Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.
35Hunipa ngao yako ya ushindi, nao mkono wako wa kuume hunitegemeza, unajishusha chini ili kuniinua.
36Huyapanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze.