36Huyapanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze.
37Niliwafuatia adui zangu na nikawapata, sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.
38Niliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena; walianguka chini ya miguu yangu.
39Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.
40Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, nami nikawaangamiza adui zangu.