43Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu; umenifanya kuwa kiongozi wa mataifa, watu ambao sikuwajua wananitumikia.
44Mara wanisikiapo hunitii, wageni hunyenyekea mbele yangu.
45Wote wanalegea, wanatoka katika ngome zao wakitetemeka.
46Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu!
47Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, awatiishaye mataifa chini yangu,