5Walikulilia wewe na ukawaokoa, walikutegemea wewe nao hawakuaibika.
6Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau.
7Wote wanionao hunidhihaki, hunivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao:
8Husema, “Anamtegemea Bwana, basi Bwana na amwokoe. Amkomboe basi, kwa maana anapendezwa naye.”
9Hata hivyo ulinitoa tumboni, ukanifanya nikutegemee, hata nilipokuwa ninanyonya matiti ya mama yangu.