4Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao, walikutumaini nawe ukawaokoa.
5Walikulilia wewe na ukawaokoa, walikutegemea wewe nao hawakuaibika.
6Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau.
7Wote wanionao hunidhihaki, hunivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao:
8Husema, “Anamtegemea Bwana, basi Bwana na amwokoe. Amkomboe basi, kwa maana anapendezwa naye.”