2Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu, hata usiku, sinyamazi.
3Hata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Uliye Mtakatifu; wewe ni sifa ya Israeli.
4Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao, walikutumaini nawe ukawaokoa.
5Walikulilia wewe na ukawaokoa, walikutegemea wewe nao hawakuaibika.
6Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau.