1Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa? Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu?
2Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu, hata usiku, sinyamazi.
3Hata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Uliye Mtakatifu; wewe ni sifa ya Israeli.
4Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao, walikutumaini nawe ukawaokoa.