11Nifundishe njia yako, Ee Bwana, niongoze katika njia iliyonyooka kwa sababu ya watesi wangu.
12Usiniachilie kwa nia za adui zangu, kwa maana mashahidi wa uongo wameinuka dhidi yangu, wakipumua ujeuri.
13Nami bado nina tumaini hili: nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai.
14Mngojee Bwana, uwe hodari na mwenye moyo mkuu, nawe, umngojee Bwana.