3Sauti ya Bwana iko juu ya maji; Mungu wa utukufu hupiga radi, Bwana hupiga radi juu ya maji makuu.
4Sauti ya Bwana ina nguvu; sauti ya Bwana ni tukufu.
5Sauti ya Bwana huvunja mierezi; Bwana huvunja vipande vipande mierezi ya Lebanoni.
6Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama, Sirioni urukaruke kama mwana nyati.
7Sauti ya Bwana hupiga kwa miali ya umeme wa radi.