7Malaika wa Bwana hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa.
8Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia.
9Mcheni Bwana enyi watakatifu wake, kwa maana wale wamchao hawapungukiwi na chochote.
10Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao Bwana hawatakosa kitu chochote kilicho chema.
11Njooni, watoto wangu, mnisikilize, nitawafundisha kumcha Bwana.