18Bwana anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele.
19Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia wingi wa vitu.
20Lakini waovu wataangamia: Adui za Bwana watakuwa kama uzuri wa mashamba, watatoweka, watatoweka kama moshi.
21Waovu hukopa na hawalipi, bali wenye haki hutoa kwa ukarimu.
22Wale wanaobarikiwa na Bwana watairithi nchi, bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali.