Zaburi 37

Bwana anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele.

Psalm 37:18 (UKJV) The LORD knows the days of the upright: and their inheritance shall be for ever.

16Bora kidogo walicho nacho wenye haki kuliko wingi wa mali wa waovu wengi;

17kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa, lakini Bwana humtegemeza mwenye haki.

18Bwana anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele.

19Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia wingi wa vitu.

20Lakini waovu wataangamia: Adui za Bwana watakuwa kama uzuri wa mashamba, watatoweka, watatoweka kama moshi.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.