34Mngojee Bwana, na uishike njia yake. Naye atakutukuza uirithi nchi, waovu watakapokatiliwa mbali, utaliona hilo.
35Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi kama mwerezi wa Lebanoni,
36lakini alitoweka mara na hakuonekana, ingawa nilimtafuta, hakupatikana.
37Watafakari watu wasio na hatia, wachunguze watu wakamilifu, kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.
38Lakini watenda dhambi wote wataangamizwa, mafanikio yao yatakatiliwa mbali.