4Jifurahishe katika Bwana naye atakupa haja za moyo wako.
5Mkabidhi Bwana njia yako, mtumaini yeye, naye atatenda hili:
6Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko, na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri.
7Tulia mbele za Bwana na umngojee kwa uvumilivu; usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, wanapotekeleza mipango yao miovu.
8Epuka hasira na uache ghadhabu, usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu.