2kwa maana kama majani watanyauka mara, kama mimea ya kijani watakufa mara.
3Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema; Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.
4Jifurahishe katika Bwana naye atakupa haja za moyo wako.
5Mkabidhi Bwana njia yako, mtumaini yeye, naye atatenda hili:
6Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko, na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri.