1Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu, wala usiwaonee wivu watendao mabaya,
2kwa maana kama majani watanyauka mara, kama mimea ya kijani watakufa mara.
3Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema; Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.
4Jifurahishe katika Bwana naye atakupa haja za moyo wako.