Zaburi 37

Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.

Psalm 37:9 (UKJV) For evildoers shall be cut off: but those that wait upon the LORD, they shall inherit the earth.

7Tulia mbele za Bwana na umngojee kwa uvumilivu; usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, wanapotekeleza mipango yao miovu.

8Epuka hasira na uache ghadhabu, usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu.

9Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.

10Bado kitambo kidogo, nao waovu hawataonekana, ingawa utawatafuta, hawataonekana.

11Bali wanyenyekevu watairithi nchi na wafurahie amani tele.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.