7Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja: imeandikwa kunihusu katika kitabu.
8Ee Mungu wangu, natamani kuyafanya mapenzi yako; sheria yako iko ndani ya moyo wangu.”
9Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, sikufunga mdomo wangu, Ee Bwana, kama ujuavyo.
10Sikuficha haki yako moyoni mwangu; ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha upendo wako na kweli yako mbele ya kusanyiko kubwa.
11Ee Bwana, usizuilie huruma zako, upendo wako na kweli yako daima vinilinde.