Zaburi 44

je, Mungu hangaligundua hili, kwa kuwa anazijua siri za moyo?

Psalm 44:21 (UKJV) Shall not God search this out? for he knows the secrets of the heart.

19Lakini ulituponda na kutufanya makao ya mbweha, na ukatufunika kwa giza nene.

20Kama tungalikuwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kunyooshea mikono yetu kwa mungu mgeni,

21je, Mungu hangaligundua hili, kwa kuwa anazijua siri za moyo?

22Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.

23Amka, Ee Bwana! Kwa nini unalala? Zinduka! Usitukatae milele.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.