3Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu.
4Nitatega sikio langu nisikilize mithali, nitafafanua kitendawili kwa zeze:
5Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja, wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka,
6wale wanaotegemea mali zao na kujivunia utajiri wao mwingi?
7Hakuna mwanadamu awaye yote awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake.