1Sikieni haya, enyi mataifa yote, sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii.
2Wakubwa kwa wadogo, matajiri na maskini pamoja:
3Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu.
4Nitatega sikio langu nisikilize mithali, nitafafanua kitendawili kwa zeze:
5Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja, wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka,