14Toa sadaka za shukrani kwa Mungu, timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana,
15na uniite siku ya taabu; nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”
16Lakini kwake mtu mwovu, Mungu asema: “Una haki gani kunena sheria zangu au kuchukua agano langu midomoni mwako?
17Unachukia mafundisho yangu na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
18Unapomwona mwizi, unaungana naye, unapiga kura yako pamoja na wazinzi.