15na uniite siku ya taabu; nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”
16Lakini kwake mtu mwovu, Mungu asema: “Una haki gani kunena sheria zangu au kuchukua agano langu midomoni mwako?
17Unachukia mafundisho yangu na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
18Unapomwona mwizi, unaungana naye, unapiga kura yako pamoja na wazinzi.
19Unakitumia kinywa chako kwa mabaya na kuuongoza ulimi wako kwa hila.