Zaburi 68

Bali wenye haki na wafurahi, washangilie mbele za Mungu, wafurahi na kushangilia.

Psalm 68:3 (UKJV) But let the righteous be glad; let them rejoice before God: yea, let them exceedingly rejoice.

1Mungu na ainuke, watesi wake watawanyike, adui zake na wakimbie mbele zake.

2Kama vile moshi upeperushwavyo na upepo, vivyo hivyo uwapeperushe mbali, kama vile nta iyeyukavyo kwenye moto, vivyo hivyo waovu na waangamie mbele za Mungu.

3Bali wenye haki na wafurahi, washangilie mbele za Mungu, wafurahi na kushangilia.

4Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake, mtukuzeni yeye aendeshwaye juu ya mawingu: jina lake ni Bwana, furahini mbele zake.

5Baba wa yatima, mtetezi wa wajane, ni Mungu katika makao yake matakatifu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.