29Kwa sababu ya Hekalu lako Yerusalemu wafalme watakuletea zawadi.
30Mkemee mnyama aliyeko kwenye manyasi, kundi la mafahali katikati ya ndama za mataifa. Na walete minara ya madini ya fedha wakinyenyekea. Tawanya mataifa yapendayo vita.
31Wajumbe watakuja kutoka Misri, Kushi atajisalimisha kwa Mungu.
32Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia, mwimbieni Bwana sifa,
33mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, yeye angurumaye kwa sauti kuu.