31Wajumbe watakuja kutoka Misri, Kushi atajisalimisha kwa Mungu.
32Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia, mwimbieni Bwana sifa,
33mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, yeye angurumaye kwa sauti kuu.
34Tangazeni uwezo wa Mungu, ambaye fahari yake iko juu ya Israeli, ambaye uwezo wake uko katika anga.
35Ee Mungu, wewe unatisha katika mahali patakatifu pako, Mungu wa Israeli huwapa watu wake uwezo na nguvu. Mungu Asifiwe!