15Usiache mafuriko yanigharikishe au vilindi vinimeze, au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu.
16Ee Bwana, unijibu, kwa wema wa upendo wako; kwa huruma zako nyingi unigeukie.
17Usimfiche mtumishi wako uso wako, uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida.
18Njoo karibu uniokoe, nikomboe kwa sababu ya adui zangu.
19Unajua jinsi ninavyodharauliwa, kufedheheshwa na kuaibishwa, adui zangu wote unawajua.