7Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, aibu imefunika uso wangu.
8Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe.
9Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia.
10Ninapolia na kufunga, lazima nivumilie matusi.
11Ninapovaa nguo ya gunia, watu hunidharau.