Zaburi 74

Kwa nini unazuia mkono wako, mkono wako wa kuume? Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako na uwaangamize!

Psalm 74:11 (UKJV) Why withdraw you your hand, even your right hand? pluck it out of your bosom.

9Hatukupewa ishara za miujiza; hakuna manabii waliobaki, hakuna yeyote kati yetu ajuaye hali hii itachukua muda gani.

10Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini? Je, adui watalitukana jina lako milele?

11Kwa nini unazuia mkono wako, mkono wako wa kuume? Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako na uwaangamize!

12Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani, unaleta wokovu duniani.

13Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako; ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.