13Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako; ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji.
14Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani nawe ukamtoa kama chakula kwa viumbe vya jangwani.
15Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito, ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima.
16Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia, uliziweka jua na mwezi.
17Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia, ulifanya kiangazi na masika.