6nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku. Moyo wangu ulitafakari na roho yangu ikauliza:
7“Je, Bwana atakataa milele? Je, hatatenda mema tena?
8Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele? Je, ahadi yake imekoma nyakati zote?
9Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, katika hasira amezuia huruma yake?”
10Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: lakini nitakumbuka miaka ya mkono wa kuume wa Aliye Juu Sana.”