28Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao, kuzunguka mahema yao yote.
29Walikula na kusaza, kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani.
30Kabla hawajamaliza kula walichokitamani, hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao,
31hasira ya Mungu ikawaka juu yao, akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao, akiwaangusha vijana wa Israeli.
32Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi, licha ya maajabu yake, hawakuamini.