20Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, na nimemtia mafuta yangu matakatifu.
21Kitanga changu kitamtegemeza, hakika mkono wangu utamtia nguvu.
22Hakuna adui atakayemtoza ushuru, hakuna mtu mwovu atakayemwonea.
23Nitawaponda adui zake mbele zake na kuwaangamiza watesi wake.
24Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye, kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa.