30“Kama wanae wataacha amri yangu na wasifuate sheria zangu,
31kama wakihalifu maagizo yangu na kutoshika amri zangu,
32nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo, uovu wao kwa kuwapiga,
33lakini sitauondoa upendo wangu kwake, wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.
34Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.