11Tutakufanyia vipuli vya dhahabu, vyenye kupambwa kwa fedha.
12Wakati mfalme alipokuwa mezani pake, manukato yangu yalisambaza harufu yake nzuri.
13Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemane kati ya matiti yangu.
14Mpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada cha maua ya mhina kutoka mashamba ya mizabibu ya En-Gedi.
15Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Tazama jinsi ulivyo mzuri! Macho yako ni kama ya hua.